Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa gaidi wa kikundi cha Daesh ambaye ni raia wa Saudi Arabia imetangazwa na vyombo vya habari nchini Syria.
Abu Hudhaifah Al Jazrawiy ni katika magaidi wanaotoka katika nchi ya Saudi Arabia ambapo aliojiounga na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria hata kufikia leo ameangamia nchini humo kutokana na mashambulizi ya anga ya majeshi ya Syria yalioshambulia msafara wa magaidi hao katika mkoa wa Raqqah.
Gaidi huyo alikuwa ni katika wachinjaji wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ambapo mara kadhaa alishuhudiwa akiwachinja wananchi wa Iraqi katika mikoa mbalimbali inayokaliwa na magaid hao nchini Iraq.
Maelfu ya wananchi wa Saudi Arabia walimiminika nchini Syria kwaajili ya kujiunga na vikundi mbalimbali vya kigaidi nchini humo hususan kikundi cha Daesh ambapo mpaka sasa wengi kati yao wameangamizwa na majeshi ya serikali ya Syria.
Mkoa wa Raqqah ndio mji mkuu wa uongozi wa kigaidi wa Daesh nchini Syria ambapo wamekusanyika maelfu ya magaidi wa kikundi hicho kutoka nchi mbalimbali duniani katika kutekeleza mipango ya kigaidi nchini Syria.
mwisho wa Habari/290